• HABARI MPYA

  Monday, June 14, 2021

  UHOLANZI YAICHAPA UKRAINE 3-2 AMSTERDAM EURO 2020

  UHOLANZI imeanza vyema Euro 2020 baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Ukraine katika mchezo wa Kundi C jana Uwanja wa Johan Cruijff Arena Jijini Amsterdam.
  Mabao ya Uholanzi yalifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 52, Wout Weghorst dakika ya 58 na Denzel Dumfries dakika ya 85, wakati ya Ukraine yalifungwa na Andrii Yarmolenko dakika ya 75 na Roman Yaremchuk dakika ya 79.
  Nayo Austria iliichapa 3-1 Macedonia Kaskazini katika mchezo wa Kundi C Uwanja wa Taifa wa in Bucharest nchini Romania, wakati England iliichapa Croatia 1-0 Uwanja wa Wembley.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UHOLANZI YAICHAPA UKRAINE 3-2 AMSTERDAM EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top