• HABARI MPYA

  Saturday, June 19, 2021

  MTIBWA SUGAR WATWAA UBINGWA WA LIGI YA VIJANA U20 KWA MARA YA TATU MFULULIZO BAADA YA KUICHAPA YANGA 2-1

   TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Yanga SC katika fainali usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Mtibwa Sugar inayofundishwa na Awadh Juma yamefungwa na Omary Marungu kwa penalti dakika ya 10 na Richard Mwamba dakika ya 24, wakati la Yanga limefungwa na Abdulkarim Yunus dakika ya 82.
  Mchezo ulisimama kwa muda dakika ya 88 baada ya refa kukataa bao la Yanga lililofungwa na Abdulkarim Yunus ambalo lingekuwa la kusawazisha.


  Ikumbukwe Simba SC imefanikiwa kupata nafasi ya tatu baada ya ushindi wa penalti 4-1 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 jioni ya leo.
  Mtibwa Sugar imetoa Mchezaji Bora na Kiungo Bora wa Mashindano, Joseph Mkele, Mfungaji Bora Omary Marungu aliyefunga mabao sita, Kocha Awadh Juma, wakati Yanga imetoa Kipa Bora, Geoffrey Magaigwa na Beki Bora Ally Mohamed Said.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WATWAA UBINGWA WA LIGI YA VIJANA U20 KWA MARA YA TATU MFULULIZO BAADA YA KUICHAPA YANGA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top