• HABARI MPYA

  Wednesday, June 16, 2021

  UFARANSA YAILAZA UJERUMANI 1-0 MUNICH EURO 2020

   BAO la kujifunga la beki Mats Hummels dakika ya 20 limewapa Ufaransa ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ujerumani katika mchezo wa Kundi F Euro 2020 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Ureno imeshinda 3-0 dhidi ya wenyeji, Hungary Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest.
  Mabao ya mabingwa hao watetezi yamefungwa na Raphaël Guerreiro dakika ya 84 na Nahodha Cristiano Ronaldo dakika ya 87 kwa penalti na 90 na ushei akimalizia pasi ya Rafa Silva.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UFARANSA YAILAZA UJERUMANI 1-0 MUNICH EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top