• HABARI MPYA

  Saturday, June 26, 2021

  SIMBA SC YAICHAPA AZAM FC 1-0 NA KUITUPA NJE ASFC, KUKUTANA NA YANGA SC KATIKA FAINALI JULAI 25 KIGOMA

  MABINGWA watetezi, Simba SC wamefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo, kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone dakika ya 90 na ushei akimalizia mpira wa adhabu alioanzishiwa na winga Mghana, Bernard Morrison baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa nje kidogo ya boksi upande wa kulia.
  Sasa Simba SC watakutana na watani wao wa jadi, Yanga SC katika fainali Julai 25 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma kuwania taji la tatu mfululizo la Azam Sports Federation Cup (ASFC).


  Ikumbukwe jana Yanga SC iliitoa Biashara United ya Mara kwa kuichapa 1-0 pia, bao pekee la mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA AZAM FC 1-0 NA KUITUPA NJE ASFC, KUKUTANA NA YANGA SC KATIKA FAINALI JULAI 25 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top