• HABARI MPYA

  Monday, June 14, 2021

  YANGA SC YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA VIJANA U20 BAADA YA KUICHAPA MWADUI FC 3-0 UWANJA WA CHAMAZI

   TIMU ya Yanga imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo wa Kundi A, mabao ya Yanga B inayofundishwa na Said Maulid 'SMG' yamefungwa na Abby Mikimba dakika ya 12 na Abdulkarim Yunus mawili, dakika ya 44 na 48.
  Yanga SC imemaliza mechi tatu za Kundi A na pointi saba, ikishinda mbili, nyingine 2-0 dhidi ya JKT Tanzania na sare ya bila kufungana na watani wao wa jadi, Simba.
  Maana yake wanatinga Nusu Fainali ya michuano hiyo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA VIJANA U20 BAADA YA KUICHAPA MWADUI FC 3-0 UWANJA WA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top