• HABARI MPYA

  Saturday, June 19, 2021

  UFARANSA YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA HUNGARY JIJINI BUDAPEST

  UFARANSA wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Hungary katika mchezo wa Kundi F Euro 2020 leo Uwanja wa Puskas Arena Jijini Budapest.
  Hungary walitangulia kwa bao la beki wa Fehervar, Attila Fiola dakika ya 45 na ushei, kabla ya mshambuliaji wa Barcelona, Antoine Griezmann kuisawazishia Ufaransa dakika ya 66.
  Ufaransa inafikisha pointi nne baada ya mechi mbili na kupanda kileleni japo kwa muda, ikiizidi pointi moja Ureno inayomenyana na Ujerumani muda huu, wakati Hungary leo imeokota pointi ya kwanza. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UFARANSA YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA HUNGARY JIJINI BUDAPEST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top