• HABARI MPYA

  Tuesday, June 22, 2021

  TANZANIA PRISONS YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA COASTAL UNION LEO SUMBAWANGA

  TANZANIA Prisons imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Samson Mbangula dakika ya 19 na Jeremiah Juma dakika ya 36, wakati ya Coastal Union yamefungwa na Abdul Suleiman kwa penalti dakika ya 23 na Mudathir Said dakika ya 85.
  Kwa matokeo hayo Prisons inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 32 na kusogea nafasi ya saba kutoka ya tisa, wakati Coastal inafikisha pointi 34 za mechi 31 sasa, ingawa inabako nafasi ya 16 katika ligi ya timu 18 ambayo mwishoni mwa msimu tatu zitashuka.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA COASTAL UNION LEO SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top