• HABARI MPYA

  Wednesday, June 16, 2021

  RONALDO APIGA MBILI URENO YAICHAPA HUNGARY 3-0

  URENO imeanza vyema Euro 2020 baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Hungary katika mchezo wa Kundi F usiku huu Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest.
  Mabao ya mabingwa hao watetezi yamefungwa na Raphaël Guerreiro dakika ya 84 na Nahodha Cristiano Ronaldo dakika ya 87 ka penalti na 90 na ushei akimalizia pasi ya Rafa Silva.
  Ronaldo anakuwa mfungaji wa mabao mengi kihistoria kwenye fainali za Kombe hilo la Mataifa ya Ulaya, 11 akimpiku Mfaransa Michel Platini.  Wakati Platini alifunga mabao yake yote kwenye fainali za mwaka 1984 pekee, Ronaldo amefunga kwenye fainali tano tofauti.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Ufafansa imewafunga wenyeji,  Ujerumani 1-0, bao la kujifunga la beki Mats Hummels dakika ya 20 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO APIGA MBILI URENO YAICHAPA HUNGARY 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top