• HABARI MPYA

  Tuesday, June 15, 2021

  BIASHARA UNITED YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA 1-1 NA NAMUNGO FC MUSOMA LEO KATIKA LIGI KUU

   TIMU ya Biashara United imelazimishwa sare ya 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Lenny David Kisu alianza kujifungia dakika ya tatu tu kuipatia Namungo FC bao la kuongoza, kabla ya Dennis Nkane kuisawazishia Biashara United dakika moja tu baadaye.
  Kwa matokeo hayo, Biashara United inafikisha pointi 46 baada ya kucheza mechi 31, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa pointi 14 na Azam FC, wakati Namungo FC inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 31 na kusogea nafasi ya tano.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA 1-1 NA NAMUNGO FC MUSOMA LEO KATIKA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top