• HABARI MPYA

  Wednesday, June 16, 2021

  WILDER AGOMA KUZUNGUMZA UTAMBULISHO PAMBANO NA FURY

  BONDIA Mmarekani, Deontay "The Bronze Bomber" Wilder aligeuka bubu wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari na mpinzani wake, bingwa wa WBC uzito wa juu Tyson "The Gypsy King" Fury Jijini Los Angeles kuelekea pambano lao la tatu Julai 24 ukumbi wa T-Mobile Arena, Jijini Las Vegas, Marekani. 
  Mmarekani huyo, Wilder alikuwa amevaa headphones wakati wote wa mkutano na alikataa hata kujibu maswali ya waandishi wa habari na hakusema chochote hata walipoinuka kutazamana uso kwa uso kwa dakika zote tano alikuwa kimya.
  Muingereza Fury alimpiga kwa TKO raundi ya saba Wilder Jijini Las Vegas Februari mwaka jana na kumpoka taji la WBC, hilo likiwa pambano la pili baina yao kufuatia Desemba mwaka 2018 lililomalizika kwa droo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WILDER AGOMA KUZUNGUMZA UTAMBULISHO PAMBANO NA FURY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top