• HABARI MPYA

  Sunday, June 13, 2021

  LUKAKU AFUNGA MAWILI UBELGIJI YAICHAPA URUSI 3-0

  MSHAMBULIAJI wa Inter Milan ya Italia, Romelu Lukaku jana amefunga mabao mawili dakika ya 10 na 88, Ubelgiji ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Urusi bao lingine likifungwa na beki wa Borussia Dortmund, Thomas Meunier dakika ya 34 katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Saint-Petersburg Jijini St. Petersburg.
  Naye kiungo wa Denmark, Christian Eriksen jana alikimbizwa hospitali jana baada ya kuzimia Uwanja wa Parken Jijini Copenhagen wakati wa mchezo wa Kundi B Euro dhidi ya Finland.
  UEFA ilisitisha mechi hiyo baada ya tukio hilo, kabla ya kuamuru iendelee kufuata hali ya Eriksen kuimarika hospitali ambako imeripotiwa anaendelea vizuri – na Finland wakaibuka na ushindi wa 1-0, bao pekee la mshambuliaji wa Union Berlin ya Ujerumani, Joel Pohjanpalo dakika ya 59.


  Mechi nyingine za jana, bao la dakika ya 74 la mshambuliaji wa Cardiff City ya England, Kieffer Moore liliisaidia Wales kupata sare ya 1-1 na Uswisi iliyotangulia kwa bao la mshambuliaji mzaliwa wa Cameroon, Breel-Donald Embolo anayechezea Borussia Monchengladbach dakika ya 49 katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Baki Olimpiya Jijini Baku.
  Naye mshambuliaji wa Inter Milan ya Italia, Romelu Lukaku akafunga mabao mawili dakika ya 10 na 88, Ubelgiji ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Urusi bao lingine likifungwa na beki wa Borussia Dortmund, Thomas Meunier dakika ya 34 katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Saint-Petersburg Jijini St. Petersburg.
  Euro 2020 zinaendelea leo kwa mechi tatu, ikiwemo England kuwakaribisha Croatia kuanzia Saa 10:00 jioni katika mchezo wa Kundi D Uwanja Wembley Jijini London, Macedonia Kaskazini dhidi ya Austria Uwanja wa Taifa wa Bucureşti na Saa 1:00 usiku na Uholanzi dhidi ya Ukraine Saa 4:00 usiku Uwanja wa Johan Cruijff Arena Jijini Amsterdam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AFUNGA MAWILI UBELGIJI YAICHAPA URUSI 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top