• HABARI MPYA

  Thursday, June 17, 2021

  KIPA METACHA MNATA ASIMAMISHWA YANGA SC BAADA YA KUWAONYESHA ISHARA YA MATUSI MASHABIKI LEO UWANJANI


  KLABU ya Yanga imemsimamisha kipa wake namba moja, Metacha Boniphace Mnata kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.
  Mashabiki wa Yanga walikerwa na kitendo cha Mnata kuruhusu mabao mawili rahisi timu ikishinda 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Na wakati anatolewa uwanjani kwa msaada wa askari Polisi kumuepusha na mikono ya mashabiki wenye hasira waliokuwa wanamtolewa maneno makali na kumtupia chupa, kipa huyo akawaonyesha ishara ya kuwatusi.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA METACHA MNATA ASIMAMISHWA YANGA SC BAADA YA KUWAONYESHA ISHARA YA MATUSI MASHABIKI LEO UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top