• HABARI MPYA

  Friday, June 18, 2021

  IDDI NADO NA MPIANA MONZINZI KILA MMOJA AFUNGA MABAO MAWILI AZAM FC YAICHAPA GWAMBINA FC 4-1 CHAMAZI

   WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Gwambina FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex. Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Mpiana Monzinzi dakika ya 32 na 57 na kiungo Mzawa, Iddi Suleiman 'Nado' dakika ya 55 na 74, wakati la Gwambina FC limefungwa na Baraka Mtuwi dakika ya 38.
  Kwa ushindi huo, Azam FC imefikisha pointi 63 baada ya kucheza mechi 31, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na vigogo, Yanga SC ambao pia wana mechi moja mkononi.


  Gwambina FC inabaki na pointi zake 31 za mechi 31 sasa katika nafasi ya 17, nafasi ya pili kutoka chini kati ya tatu za kushuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IDDI NADO NA MPIANA MONZINZI KILA MMOJA AFUNGA MABAO MAWILI AZAM FC YAICHAPA GWAMBINA FC 4-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top