• HABARI MPYA

  Wednesday, June 16, 2021

  KAGERA SUGAR WAICHAPA TANZANIA PRISONS BAO 1-0 KAITABA, JKT NAYO YAILAZA IHEFU SC 2-0 DODOMA

  WENYEJI, Kagera Sugar wameichapa Tanzania Prisons bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji Yussuf Mhilu dakika ya 44 na kwa ushindi huo, Kagera Sugar wanafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 31 na kusogea nafasi ya 11 kutka ya 15, wakati Tanzania Priosns inabaki na pointi zake 41 za mechi 31 katika nafasi ya nane.
  Nayo JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


  Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Jabir Aziz dakika ya nne na Edson Katanga dakika ya nane na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 31 na kupanda nafasi ya 12 kutoka ya 15, wakati Ihefu SC inashukia nafasi ya 14 kutoka ya 12 ikibaki na pointi zake 34 za mechi 31 sasa.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR WAICHAPA TANZANIA PRISONS BAO 1-0 KAITABA, JKT NAYO YAILAZA IHEFU SC 2-0 DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top