• HABARI MPYA

  Wednesday, June 23, 2021

  HISPANIA NA SWEDEN ZATINGA 16 BORA EURO 2020, LEWANDOWSKI NJE

  HISPANIA imefuzu Hatua ya 16 Bora baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Slovakia katika mchezo wa Kundi E wa Euro 2020 leo Uwanja wa Olímpico Jijini Sevilla.
  Mabao ya Hispania yamefungwa na Martin Dúbravka aliyejifunga dakika ya 30, Aymeric Laporte dakika ya 45, Pablo Sarabia dakika ya 56, Ferran Torres dakika ya 67 na Juraj Kucka aliyejifunga dakika ya 71.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Sweden imeichapa Poland 3-2 Uwanja wa Saint-Petersburg Jijini St. Petersburg, Urusi.


  Mabao ya Sweden yamefungwa na Emil Forsberg mawili dakika ya pili na 59 na Viktor Claesson dakika ya 90 na ushei, wakati ya Poland yote yamefungwa na Robert Lewandowski dakika ya 61 na 84.
  Sweden inamaliza kileleni na pointi zake saba, ikifuatiwa na Hispania pointi tano na zote zinafuzu 16 Bora ya michuano hiyo, wakati Slovakia iliyomaliza na pointi tatu na Poland pointi moja zote zinaaga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HISPANIA NA SWEDEN ZATINGA 16 BORA EURO 2020, LEWANDOWSKI NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top