• HABARI MPYA

  Monday, June 28, 2021

  BRAZIL YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA MAKUNDI KWA SARE COPA AMERICA

  WENYEJI, Brazil wamekamilisha mechi zao za Kundi B Copa America kwa sare ya 1-1 na Ecuador usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Olímpico Pedro Ludovico Teixeira huko Goiânia, Goiás.
  Wenyeji walitangulia kwa bao la Éder Militão dakika ya 37 akimalizia pasi ya Éverton, kabla ya Ángel Mena kuisawazishia Ecuador dakika ya 53 akimalizia pasi ya Enner Valencia.
  Mechi nyingine ya kundi hilo jana, Peru Venezuela 1-0, bao pekee la André Carrillo Uwanja wa Taifa wa Brasília.
  Brazil imemaliza kileleni mwa Kundi B kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Peru pointi saba, Colombia nne, Ecuador tatu na zote zimetinga Robo Fainali, wakati Venezuela iliyoshika mkia kwa pointi zake mbili imeaga mashindano.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRAZIL YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA MAKUNDI KWA SARE COPA AMERICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top