• HABARI MPYA

  Friday, June 04, 2021

  AZAM FC YAMTIA PINGU NYOTA WAKE MWINGINE, YAMSAINISHA AYOUB LYANGA MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI ATADUMU CHAMAZI HADI 2024

  KLABU ya Azam FC imemuongezea mkataba mpya wa miaka miwili na kiungo wake mshambuliaji, Ayoub Lyanga.
  Zoezi la kuingia mkataba huo baina mchezaji huyo limesimamiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu, Abdulkarim Amin 'Popat'.
  Lyanga aliyejiunga na Azam msimu huu akitokea Coastal Union ya Tanga ataendelea kusalia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2024.


  Katika msimu wake huu wa kwanza, Lyanga amechangia mabao 10 ndani ya Azam FC kwenye mashindano yote hadi sasa akiwa amefunga mabao saba na kutoa pasi mbili za mwisho za mabao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huku akitupia moja katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMTIA PINGU NYOTA WAKE MWINGINE, YAMSAINISHA AYOUB LYANGA MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI ATADUMU CHAMAZI HADI 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top