• HABARI MPYA

  Thursday, June 03, 2021

  NAHODHA WA ZAMANI WA TAIFA STARS, ALLY MAYAY TEMBELE AENGULIWA UCHAGUZI WA CHAMA CHA WACHEZAJI ETI HAKIDHI VIGEZO VYA KATIBA


  NAHODHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Ally Mayay Tembele ameenguliwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA) kwa madai ya kutokidhi vigezo vya Katiba.
  Taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema Mayay ameenguliwa kwa sababu hajatelekeza Ibara ya 27 (6) ya Katiba ya SPUTANZA.
  Kamati hiyo imempitisha mchezaji mwingine wa zamani wa Yanga SC, Abeid Mohamed Mziba pekee kuwania Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kupitia SPUTANZA baada ya usaili uliofanyika Mei 31.


  Uchaguzi wa SPUTANZA unatarajiwa kufanyika Juni 19, mwaka huu.

  Ally Mayay Tembele (katikati) enzi zake akiichezea timu ya taifa mwaka 1999
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAHODHA WA ZAMANI WA TAIFA STARS, ALLY MAYAY TEMBELE AENGULIWA UCHAGUZI WA CHAMA CHA WACHEZAJI ETI HAKIDHI VIGEZO VYA KATIBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top