• HABARI MPYA

  Friday, June 11, 2021

  AZAM FC YAMUONGEZEA MKATABA BRYSON RAPHAEL HADI 2O23 NA KUMSAJILI BEKI WA RUVU SHOOTING EDWARD CHARLES MANYAMA

   KLABU ya Azam FC imemuongeza mkataba wa miaka miwili kiungo wake mkabaji, Bryson Raphael, huku pia ikimsajili beki wa Ruvu Shooting, Edward Charles Manyama.
  Bryson amekuwa na kiwango kizuri msimu huu, akisifika kwa kasi yake ya ukabaji.
  Kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania, kwa kusaini mkataba huo mpya ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023.


  Naye Manyama, amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Azam FC kuanzia msimu ujao 2021/22 hadi 2023/24.
  Azam FC pia imefanikiwa kufikia makubaliano na klabu yake, Ruvu Shooting ambayo imeridhia kijana akafanye kazi Chamazi.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMUONGEZEA MKATABA BRYSON RAPHAEL HADI 2O23 NA KUMSAJILI BEKI WA RUVU SHOOTING EDWARD CHARLES MANYAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top