• HABARI MPYA

  Saturday, June 19, 2021

  ENGLAND NA CROATIA ZOTE ZALAZIMISHWA SARE EURO 2020

  TIMU ya taifa ya England imelazimishwa sare ya bila kufungana na Scotland katika mchezo wa Kundi D usiku huu Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Croatia imetoa sare ya 1-1 na Jamhuri ya Czech Uwanja wa Hampden Park Jijini Glasgow.
  Sasa Czech na England kila moja ina pointi nne baada ya mechi mbili kwanza, wakati Scotland na Croatia kila moja ina pointi moja.
  Katika mchezo wa Kundi E, Sweden imeshinda 1-0 dhidi ya Slovakia Uwanja wa Saint-Petersburg Jijini Saint-Petersburg.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ENGLAND NA CROATIA ZOTE ZALAZIMISHWA SARE EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top