• HABARI MPYA

  Sunday, June 20, 2021

  BIASHARA UNITED YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 MUSOMA, KAGERA SUGAR YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA IHEFU KAITABA

  BAO pekee la Abdulmajid Mangalo dakika ya 45 na ushei limewapa wenyeji, Biashara United ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Kwa ushindi huo, Biashara United inafikisha pointi 49 baada ya kucheza mechi 32, ingawa inabaki nafasi ya nne, nyuma ya Azam FC yenye pointi 63 za mechi 31, wakati JKT inabaki ma pointi zake 36 za mechi 32 sasa katika nafasi ya 14.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Ihefu SC ya Mbarali, Mbeya Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.


  Kagera Sugar inafikisha pointi 37 za mechi 32 sasa na kupanda kwa nafasi moja tu hadi ya 11, ikiwazidi wastani wa mabao tu ndugu zao, Mtibwa Sugar ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Na Ihefu SC ya kocha Zubery Katwila inafikisha pointi 35 za mechi 32 sasa, ingawa inabaki nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 MUSOMA, KAGERA SUGAR YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA IHEFU KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top