• HABARI MPYA

  Friday, June 18, 2021

  MBEYA CITY YAICHAPA COASTAL UNION 2-0 LEO MECHI YA LIGI KUU BARA UWANJA WA SOKOINE

  TIMU ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa na Juma Luizio dakika ya 18 na George Sangija dakika ya 78 na kwa ushindi huo, MCC inafikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 31 na kusogea nafasi ya 11 ikizidiwa wastani wa mabao tu na Ruvu Shooting.
  Coastal Union yenyewe inabaki nafasi ya 16, eneo kabisa la kushuka Daraja ikiwa na pointi 33 za mechi 30 sasa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA COASTAL UNION 2-0 LEO MECHI YA LIGI KUU BARA UWANJA WA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top