• HABARI MPYA

  Friday, June 25, 2021

  YANGA SC YATINGA FAINALI ASFC BAADA YA KUICHAPA BIASHARA UNITED 1-0 BAO PEKEE LA YACOUBA SOGNE TABORA

  VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United jioni ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Sogne aliyefunga bao hilo dakika ya 22 akimalizia pasi ya kiungo Mzanzibar, Feisal Salum Abdallah.
  Yanga sasa watakutana na mshindi kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na Azam FC zinazomenyana kesho katika Nusu Fainali nyingine Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATINGA FAINALI ASFC BAADA YA KUICHAPA BIASHARA UNITED 1-0 BAO PEKEE LA YACOUBA SOGNE TABORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top