• HABARI MPYA

  Friday, April 05, 2024

  COASTAL UNION YATINGA ROBÓ FAINALI KOMBE LA TFF KWA MATUTA


  TIMU ya Coastal Unión imefanikiwa kwenda Robó Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya JKT Tanzania kufuatia sare ya bila kufungana usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Coastal Union inakuwa timu ya nne kutinga Nane Bora baada ya Namungo FC, Geita Gold na Tabora United.
  Namungo FC iliitoa Kagera Sugar kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya bila kufungana Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Geita Gold iliitoa Rhino Rangers ya Tabora kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita na Tabora United iliitoa Singida Fountain Gate kwa kuichapa 3-0 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YATINGA ROBÓ FAINALI KOMBE LA TFF KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top