TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mabao yote ya Azam FC leo yamefungwa na washambuliaji wake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean-Jacques Ngita Kamanga dakika ya 36 na Jephté Kitambala Bola dakika ya 63.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 55 katika mchezo wa 26, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Simba yenye pointi 58 na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 60 kufuatia kucheza mechi 25.
Kwa upande wao Fountain Gate baada ya Korea’s mchezo huo inabaki na pointi zake 29 kufuatia kucheza mechi 26 ikibaki katika nafasi ya tisa kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.


.png)
0 comments:
Post a Comment