TIMU za Geita Gold FC na Kagera Sugar FC zimefanikiwa kurejea Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi katika mechi zao za leo kila moja ikiwa nyumbani.
Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Kengold ya Mbeya, mabao ya washambuliaji, Kassim Ibrahim Feka na Mzambia Obbrey Chola Zaninge Chirwa na beki, David Charles Luhende Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Nayo Ken Gold imeichapa Songea United ya Ruvuma 3-1 Uwanja wa shule ya Sekondari ya Nyankumbu mjini Geita – mabao yake yakifungwa na kiungo Richardson Ngodya na mshambuliaji Maulid Shaaban Juma mawili,
Kwa matokeo, Kagera Sugar inafikisha pointi 71 na kuendelea kuongoza Ligi ya Championship, ikifuatiwa na Geita Gold iliyofikisha pointi 68 baada ya mechi 28 na zote zinajihakikishia kurejea Ligi Kuu zikiwa na mechi mbili mkononi.





.png)
0 comments:
Post a Comment