WENYEJI, Coastal Union wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Robert Savilla alianza kuifungia Coastal Union dakika ya 37, kabla ya Geoffrey Luzindaze kuisawazishia Namungo FC dakika ya 62.
Kwa matokeo hayo, Coastal Union inafikisha pointi 29, ingawa inabaki nafasi ya 10 na Namungo FC inafikisha pointi 26 nayo inasalia nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16 baada ya timu hizo zote kucheza mechi 26.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.


.png)
0 comments:
Post a Comment