• HABARI MPYA

  Saturday, December 02, 2023

  UWANJA WA LITI WA SINGIDA HAUNA VIGEZO LIGI KUU


  UWANJA wa LITI uliopo Singida unaotumiwa na klabu ya Singida Fountain Gate umefungiwa kwa michezo ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kutokana na kukosa sifa.
  Hatua hiyo inakuja siku moja tu baada ya mchezo wa Ligi Kuu jana baina ya Singida Fountain Gate na JKT Tanzania uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.
  Mabao ya Singida Fountain Gate yalifungwa na Marouf Tchakei dakika ya 62 na Francy Kazadi dakika ya 75, wakati ya JKT Tanzania lilifungwa na Hassan Kapalata dakika ya 26 na Hassan Nassor Maulid dakika ya 68.
  Kwa matokeo hayo, Singida Fountain Gate inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya nne, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 16 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 12.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UWANJA WA LITI WA SINGIDA HAUNA VIGEZO LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top