• HABARI MPYA

  Friday, December 01, 2023

  SINGIDA FOUNTAIN GATE SARE 2-2 NA JKT LITI


  TIMU ya Singida Fountain Gate imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao ya Singida Fountain Gate yamefungwa na Marouf Tchakei dakika ya 62 na Francy Kazadi dakika ya 75, wakati ya JKT Tanzania yamefungwa na Hassan Kapalata dakika ya 26 na Hassan Nassor Maulid dakika ya 68.
  Kwa matokeo hayo, Singida Fountain Gate inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya nne, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 16 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA FOUNTAIN GATE SARE 2-2 NA JKT LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top