• HABARI MPYA

  Saturday, December 02, 2023

  SIMBA SC YAAMBULIA SARE YA 0-0 KWA JWANENG GALAXY BOTSWANA


  TIMU ya Simba imelazimishwa sare ya bila mabao na wenyeji,  Jwaneng Galaxy katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana.
  Wekundu wa Msimbazi walikuwa leo walikuwa wanacheza mechi ya kwanza chini ya Kocha mpya Mkuu, Mualgeria Abdelhak Benchikha na huo unakuwa mchezo wa nne jumla timu hiyo kumaliza dakika 90 bila ushindi tangu wafungwe 5-1 na mahasimu, Yanga Novemba 5, mwaka huu na kumfukuza Kocha Mbrazil, Robert Oliveira 'Robertinho'.
  Mechi zilizofuata Simba ikiwa chini ya Kocha wa makipa, Mspaniola Daniel Cadena ilitoa sare za 1-1 mfululizo, na Namungo FC Novemba 9 katika Ligi Kuu pia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika Ligi ya Mabingwa Afrika zote zikchezwa Uwanja wa Benjamin Jijini Dar es Salaam.
  Kwa upande wao,  Jwaneg Galaxy wanafikisha pointi nne kufuatia kuanza na ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Wydad Athletic Jijini Marrakech wiki iliyopita.
  Mechi zijazo, Simba watakuwa wageni wa Wydad Casablanca Desemba 9 nchini Morocco, na Jwaneng watakuwa wenyeji wa ASEC hapo hapo Francistown. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAMBULIA SARE YA 0-0 KWA JWANENG GALAXY BOTSWANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top