• HABARI MPYA

  Thursday, October 19, 2023

  WAZIRI WA MICHEZO DK. NDUMBARO ATETA NA UONGOZI WA FIFA NA CAF


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA ) katika Ukanda wa CECAFA, Andrea Silva na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Veron Mosengo - Omba kwa mazungumzo Jijini Dar es Salaam.
  Wawili hao wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya mechi ya Ufunguzi wa michuano ya African Football League (AFC) kati ya Timu ya Simba ya Tanzania na Al Alhy ya nchini Misri, utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Oktoba 20,2023.
  Katika kikao hicho viongozi hao pamoja na mambo mengine wamejadili maendeleo ya Michezo nchini ambapo kwa sasa Tanzania inafanya vizuri katika michezo hususani mchezo wa soka, kwa Timu za Taifa za wanaume na Wanawake pamoja na Ligi mbalimbali na mashindano ya Kimataifa.
  Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gerson Msigwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Neema Msitha, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na viongozi wengine wa Serikali na TFF. 
  PICHA: KIKAO CHA WAZIRI DK NDUMBARO NA VIONGOZI WA CAF, FIFA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI WA MICHEZO DK. NDUMBARO ATETA NA UONGOZI WA FIFA NA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top