• HABARI MPYA

  Sunday, October 29, 2023

  KEN GOLD YAREJEA KILELEMI LIGI YA CHAMPIONSHIP


  TIMU ya Ken Gold ya Mbeya jana imefanikiwa kupanda kileleni mwa Ligi ya NBC Championship baada ya ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. 
  Mechi nyingine za Ligi ya NBC Championship, wenyeji Pan Africans waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate Talents Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, wakati Cocpo ya Mwanza iliwalaza wenyeji, Ruvu Shooting 1-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Ushindi wa jana unafanya Ken Gold ifikishe pointi 19 na kupanda kileleni mwa Ligi ya NBC Championship, ikiwazidi pointi mbili ndugu zao, Mbeya Kwanza baada ya wote kucheza mechi nane.
  Copco imesogea nafasi ya saba baada ya kufikisha pointi 11, Pan Africans imesogea ya 13 baada ya kufikisha pointi saba, wakati Biashara United sasa ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi tisa, Ruvu Shooting yenye pointi moja inashika mkia na Fountan Gate Talents inashukia nafasi ya 12 kwa pointi zake nane baada ya wote kucheza mechi nane.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KEN GOLD YAREJEA KILELEMI LIGI YA CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top