• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2023

  VINCENT BARNABAS AREJEA YANGA KAMA KOCHA WA U20


  KLABU ya Yanga SC imemtambulisha mchezaji wake wa zamani, Vincent Barnabas Salamba kuwa kocha wake mpya Mkuu wa timu yao ya vijana chini ya umri wa miaka 20 akichukua nafasi ya Said Maulid Kalikula, pia mchezajni wa zamani wa klabu.
  Barnabas aliichezea Yanga kati ya mwaka 2008 na 2009 akitokea Kagera Sugar alikodumu kuanzia 2005 na baada ya kuachwa Jangwani akaenda African Lyon alikocheza hadi 2010 akaenda Mtibwa Sugar kumalizia soka yake kati ya 2010 na 2018 na alipostaafu akawa kocha.
  Amefundisha timu za vijana za Mtibwa Sugar kwa mafanikio akizipia ubingewa wa Ligi ya Vijana mfululizo na kutwaa tuzo za Kocha Bora wa mashindano hayo mfululizo hadi sasa anarejea Jangwani kama kocha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VINCENT BARNABAS AREJEA YANGA KAMA KOCHA WA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top