• HABARI MPYA

  Wednesday, October 04, 2023

  MAN UNITED WAMEKANDWA NA GALATASARAY PALE PALE OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wamechapwa Mabao 3-2 na Galatasaray ya Uturuki katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Galatasaray yamefungwa na Wilfried Zaha dakika ya 23, Muhammed Aktürkoğlu dakika ya 71 na Mauro Icardi dakika ya 81, wakati ya Manchester United yote yamefungwa na mshambuliaji Mdenmark, Rasmus Højlund dakika ya 17 na 67.
  Galatasaray wanafikisha pointi nne na kupanda nafasi ya pili, wakizidiwa pointi moja na Bayern Munich, wakati Manchester United ambayo haina pointi inaendelea kushika mkia nyuma ya FC Copenhagen yenye pointi moja baada ya mechi mbili za awali.
  Mchezo mwingine wa Kundi Bayern Munich waliwakanda wenyeji, FC Copenhagen 2-1 Uwanja wa Venue Parken Jjjini Copenhagen nchini Denmark.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WAMEKANDWA NA GALATASARAY PALE PALE OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top