• HABARI MPYA

  Monday, October 23, 2023

  RASMI, ZUBERI KATWILA AREJEA MTIBWA SUGAR


  RASMI Mtibwa Sugar imemtambulisha Zuberi Katwila kurejea kwenye klabu hiyo kama Kocha Mkuu kufuatia kuachana na Habib Kondo aliyeoiongoza timu kwenye mechi tano tu ikiambilia pointi mbili.
  Mechi iliyopita Mtibwa Sugar ikifungwa 2-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro timu iliongozwa na makocha Wasaidizi, Awadh Juma na Patrick Mwangata.
  Katwila anajiunga tena na Mtibwa Sugar akitokea Ihefu SC ambako aliiongoza timu katika mechi tano za msimu pia ikivuna pointi sita, kabla ya kuokota pointi ya saba juzi katika sare ya 0-0 na Coastal Unión Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.
  Mtibwa Sugar kwa sasa inashika mkia katika Ligi Kuu ya timu 16 ikiwa imeambulia sare tatu na kufungwa mechi nyingine zote tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASMI, ZUBERI KATWILA AREJEA MTIBWA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top