• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2023

  SALAH APIGA ZOTE LIVERPOOL YAICHAPA EVERTON 2-0 ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Shujaa wa Liverpool leo alikuwa ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Misri, Mohamed Salah aliyefunga mabao yote hayo, la kwanza kwa penalti dakika ya 75 na la pili dakika ya 90 akimalizia pasi ya nyota wa Uruguay, Darwin Nunez.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi moja mabingwa watetezi, Manchester City wakati Everton inabaki na pointi zake saba nafasi ya 16 ligi ya timu 18 baada ya wote kucheza mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH APIGA ZOTE LIVERPOOL YAICHAPA EVERTON 2-0 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top