• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2023

  MAKOCHA AZAM ACADEMY WAZUIA KUFANYA KAZI LIGI YA VIJANA U20


  MAKOCHA wa timu ya vijana ya Azam FC, Mohamed Badru Juma na Msaidizi wake, Mwalu Hashim Ilunga wamezuiwa kufundisha timu hiyo katika Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 iliyoanza leo Jijini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), makocha hao wote wana leseni za Diploma C za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wakati makocha wanaotakiwa kufundisha kwenye ligi hiyo ni wenye leseni za Diploma B na A za CAF.
  Aidha makocha wenye Diploma A ma B lakini wamesoma muda mrefu na hawakushiriki kozi za Maboresho hivi karibuni nao pia wamezuiwa kufundisha kwenye ligi hiyo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKOCHA AZAM ACADEMY WAZUIA KUFANYA KAZI LIGI YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top