• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2023

  AZAM ACADEMY YAANZA NA MOTO LIGI YA VIJANA U20, YANGA...


  TIMU ya Azam FC imeanza vyema Ligi ya Vijana U20 baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam Academy yamefungwa na Ashraf Kibeku moja, Mahmoud Haji matatu na Clement Richard moja pia.
  Mchezo mwingine wa leo wa Ligi Vijana U20, Yanga imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na KMC Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha TFF, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC yote yamefungwa na Maulid Tamila, wakati ya Yanga yamefungwa na Karim Shija na Henry Francis.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM ACADEMY YAANZA NA MOTO LIGI YA VIJANA U20, YANGA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top