• HABARI MPYA

  Tuesday, October 24, 2023

  SIMBA SC YAFA KIUME CAIRO, YATOLEWA KWA MABAO YA UGENINI


  TIMU ya Simba SC imetupwa nje ya michuano mipya ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali leo Uwanja wa Cairo International, Misri.
  Kiungo wa Kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute alianza kuifungia Simba dakika ya 68 akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama kabla ya mshambuliaji Mmisri, Mahmoud Abdulmonem Abdelhamid Soliman ‘Kahraba’ kuisawazishia Al Ahly dakika ya 76 akimalizia pasi ya beki Mtunisia, Ali Maâloul.
  Simba inayofundishwa na Kocha Mbrazil, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ inatolewa kwa Sheria ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Sasa Al Ahly itakutana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo imeitoa Petro de Luanda ya Angola licha ya sare ya 0-0 jana Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria – ikinufaika na ushindi wa 2-0 Ijumaa kwenye mchezo wa kwanza Jijini Luanda nchini Angola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAFA KIUME CAIRO, YATOLEWA KWA MABAO YA UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top