• HABARI MPYA

    Saturday, October 21, 2023

    SINGIDA BIG STARS YAIPIGA NAMUNGU 3-2 MAJALIWA


    TIMU ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
    Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na viungo Mkenya, Duke Ooga Abuya dakika ya 45 na ushei na Mtogo, Marouf Tchakei mawili dakika ya 68 na 81, wakati ya Namungo FC yamefungwa na Derick Mkombozi dakika ya 64 kwa penalti na Emmanuel Charles dakika ya 90 na ushei.
    Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi nane na kusogea nafasi ya sita, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake tatu nafasi ya 14 kwenye Ligi ya 16 baada ya wote kucheza mechi sita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAIPIGA NAMUNGU 3-2 MAJALIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top