• HABARI MPYA

  Thursday, October 12, 2023

  SIMBA SC YAZINDUA JEZI MPYA MAALUM KWA MICHUANO YA AFRIKA


  KUELEKEA mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Afrika (AFC) dhidi ya Al Ahly ya Misri Okotba 20, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam – Simba leo imezindua jezi maalum za michuano ya Afrika.
  Kikosi cha Simba kimeingia kambini leo kuanza kujiandaa na michuano ya CAF African Football League wakianza na mechi mbili dhidi ya mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri Oktoba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa na Oktoba 24 Uwanja wa Cairo International.
  Habari njema ni kwamba beki kipa namba moja, Aishi Manula ambaye amekuwa nje tangu Aprili mwaka jana na beki Mkongo, Henock Inonga Baka ‘Varane’ ambaye yupo nje kwa wiki mbili sasa wako fiti na Alhamisi wataanza mazoezi.
  Mchezaji majeruhi pekee aliyebaki Simba SC ni mmoja tu, kiungo Muivory Coast, Aubin Kramo Kouamé ambaye Madaktari watatazama leo ili kujua anaendeleaje.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAZINDUA JEZI MPYA MAALUM KWA MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top