• HABARI MPYA

  Wednesday, October 04, 2023

  ARSENAL YACHAPWA 2-1 UFARANSA LIGI YA MABINGWA


  WENYEJI, Lens wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa Bollaert-Delelis mjini Lens, Ufaransa.
  Mabao ya Lens yamefungwa na Adrien Thomasson dakika ya 25 na Elye Wahi dakika ya 69, wakati la Arsenal limefungwa na  Gabriel Jesus dakika ya 14.
  Kwa ushindi huo, Lens inafikisha pointi nne na kupanda kileleni ikiizidi pointi moja Arsenal baada ya wote kucheza mechi mbili.
  Mechi nyingine ya Kundi hilo, wenyeji PSV walilazimishwa sare ya 2-2 na Sevilla ya Hispania Uwanja wa Philips mjini Eindhoven, Uholanzi.
  Sevilla sasa ni ya tatu kwa pointi zake mbili, wakati PSV inaendelea kushika mkia kundini kwa pointi yake moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YACHAPWA 2-1 UFARANSA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top