• HABARI MPYA

  Sunday, October 08, 2023

  SIMBA SC YAWAKANDA SINGIDA BIG STARS 2-1 PALE PALE LITI


  TIMU ya Simba SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Singida Big Stars leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 26 na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri dakika ya 83, wakati la Singida Big Stars limefungwa na winga mzawa, Deus Kaseke dakika ya 52.
  Kwa ushindi huo, Simba inayofundishwa na Kocha Mbrazil, Robert Oliveira ‘Robertinho’ inafikisha pointi 15 na kupanda tena kileleni mwa Ligi Kuu ikiizidi pointi mbili Azam FC baada ya wote kucheza mechi tano.
  Kwa upande wao Singida Big Stars baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao tano za mechi tano sasa nafasi ya tisa kwenye Ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWAKANDA SINGIDA BIG STARS 2-1 PALE PALE LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top