• HABARI MPYA

  Monday, October 09, 2023

  ATCL NA SIMBA SC KUENDELEZA MAHUSIANO YA KIBIASHARA


  KLABU ya Simba na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) leo zimekubaliana kuendelea kushirikiana na kuipa klabu ya Simba fursa ya kutumia huduma za ATCL. 
  Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kuishukuru ATCL kwa uhusiano mzuri na Simba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula alisema, “ATCL mmekuwa washirika muhimu sana kwenye mafanikio ya Klabu ya Simba kwa kutupa usafiri wa uhakika na bora kwa ajili ya timu yetu. Tukielekea kwenye mechi ya AFL dhidi ya Al-Ahly tufurahi kujua kwamba ATCL itakuwa mbia muhimu kusafirisha mashabiki kutoka sehemu mbalimbali kuja kuangalia mchezo huo.”
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Jamal Athumani Kiggundu alisema, “ATCL inafurahi sana kuwa mbia wa Simba na iko tayari kufanya kazi pamoja na Simba katika kusafirisha timu na pia mashabiki.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ATCL NA SIMBA SC KUENDELEZA MAHUSIANO YA KIBIASHARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top