• HABARI MPYA

  Saturday, October 14, 2023

  SIMBA SC YAWATUMIA SALAM AL AHLY, YASHINDA 5-1 MECHI YA KIRAFIKI


  TIMU ya Simba SC leo imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Dar City katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji mzawa, Shaaban Iddi Chilunda mawili na viungo  Mcameroon Leandre Willy Essomba Onana, Luis Jose Miquissone kutoka Msumbiji na Mrundi, Saido Ntibanzokiza kila mmoja moja.
  Simba SC inajiandaa na michuano ya CAF African Football League ikianza na mechi mbili dhidi ya mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri Oktoba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa na Oktoba 24 Uwanja wa Cairo International.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWATUMIA SALAM AL AHLY, YASHINDA 5-1 MECHI YA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top