• HABARI MPYA

  Wednesday, October 04, 2023

  KAGERA SUGAR NA NAMUNGO FC HAKUNA MBABE, SARE 1-1


  WENYEJI. Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Kagera Sugar walitanguli kwa bao la Ally Nassor ‘Ufudu’ dakika ya 34, kabla ya Pius Buswita kuisawazishia Namungo FC dakika ya 72.
  Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi tano na kusogea nafasi ya tisa, wakati Namungo FC wanafikisha pointi tatu nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR NA NAMUNGO FC HAKUNA MBABE, SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top