• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2023

  IHEFU SC YALAZIMISHWA SULUHU NA COASTAL UNION MBARALI


  WENYEJI, Ihefu SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.   
  Kwa matokeo hayo, Ihefu SC inafikisha pointi saba na kusogea nafasi ya nane, wakati Coastal Union inafikisha pointi tatu na inabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi sita. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YALAZIMISHWA SULUHU NA COASTAL UNION MBARALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top