• HABARI MPYA

  Friday, October 27, 2023

  YANGA SC YAWACHAPA SINGIDA BIG STARS 2-0 ZOTE KAPIGA MAX


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Maxi Mpia Nzengeli aliyefunga mabao yote mawili, dakika ya 30 na 39.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 18 katika mchezo wa saba na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya Simba SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao, Singida Big Stars wanabaki na pointi zao nane na wanashuka kwa nafasi moja hadi ya 10 baada ya wao pia kucheza mechi saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAWACHAPA SINGIDA BIG STARS 2-0 ZOTE KAPIGA MAX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top