• HABARI MPYA

  Saturday, October 07, 2023

  YANGA YAZINDUKA NA KUICHAPA GEITA GOLD 3-0 KIRUMBA


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na viungo, Muivory Coast Pacome Zouazoua dakika ya 44, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 45 na ushei na Mkongo Max Mpia Nzengeli dakika ya 69.
  Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya pili, wakizidiwa pointi moja na vinara, Azam FC baada ya wote kucheza mechi tano, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake nne za mechi tano pia nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAZINDUKA NA KUICHAPA GEITA GOLD 3-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top