• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2023

  CHELSEA YATOA SARE 2-2 NA ARSENAL STAMFORD BRIDGE


  WENYEJI, Chelsea wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. 
  Chelsea ilitangulia kwa mabao ya Cole Palmer dakika ya 15 kwa penalti na Mykhailo Mudryk dakika ya 48, kabla ya Arsenal kuzinduka na mabao ya Declan Rice dakika ya 77 na Leandro Trossard dakika ya 84.
  Kwa matokeo hayo, Chelsea inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Arsenal inafikisha pointi 21 na kurejea nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao ya Mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YATOA SARE 2-2 NA ARSENAL STAMFORD BRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top